Tanzania

Vipimo vya XT

Nguvu safi.

Imara. Yenye nguvu. Kutegemeka.

XT inatumika kwenye masafa yetu yote, bila ya mfululizo wa L na programu ya injini . Kama magari yote ya Scania, anuwai ya XT itafaidika kutokana na kubadilika kwa mfumo wetu wa moduli unaojulikana sana. Inatuwezesha kupanga masuluhisho ili kukidhi mahitaji ya kibinafsi ya kila mteja ili kuhakikisha faida ya juu zaidi - kuweka viwango kila wakati, bila kukubaliana nazo.

Uthabiti wa kiwango cha juu zaidi, ufanisi wa kipekee

Injini ya Scania Super ya lita 13 inaboresha zaidi sifa yetu ya matumizi bora ya mafuta. Kupitia maboresho makubwa ya utendaji na udhibiti bora zaidi wa utoaji wa gesi ya kaboni kupitia mfumo wa Twin-SCR wa Scania, injini ya Scania Super ya lita 13 inaweka kiwango kipya cha sekta cha ubora wa usambazaji wa nishati ya breki. Hali hii inachangia kiwango cha juu zaidi cha hadi 8% cha kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji. Kiwango bora zaidi cha sekta.

Udhibiti bora zaidi wa utoaji wa gesi ya kaboni

Mfumo bora zaidi wa Twin-SCR wa Scania – wenye usambazaji mara mbili wa AdBlue – huhakikisha kiwango endelevu cha chini cha utoaji wa gesi ya kaboni katika kazi mbalimbali. Mfumo wa uendeshaji wa Super pia una sehemu ya ekzosi iliyojumuisha inayoweza kubadilishwa kwa urahisi zaidi ambayo ni nyepesi, thabiti na inatoa nafasi kubwa kati ya ardhi na fremu ya gari.

Uthabiti wa kipekee

Injini ya Scania Super ya lita 13 inatoa uthabiti wa kipekee wa kiufundi hata katika shughuli ngumu zaidi, hali ambayo inakupa muda zaidi wa matumizi ya gari, matumizi ya gari kwa muda mrefu kabla ya kufanya matengenezo na mara chache za kufanya matengenezo kuliko awali. 

Mfumo thabiti wa breki

Mfumo wa breki wa ziada wa kuachilia mbano uliojumuishwa kwenye injini (CRB), unaipa injini ya Scania Super ya lita 13 ufikiaji wa uwezo wa kushika breki za ziada wa utendaji wa juu wa hadi 350 kW, pia unatoa uwezo wa kushika breki za ziada kwa kasi ya chini iliyoboreshwa kwa ajili ya uendeshaji bora katika mandhari magumu.

Tafuta injini inayokufaa

Scania ina aina nyingi zaidi za mifumo ya injini sokoni, inayotumia dizeli na mafuta mbadala. Hali hii inarahisisha kupata injini sahihi, mfumo wa nguvu ya kuzungusha injini na uthabiti unaofaa kabisa kwa changamoto zote za kazi zako. Aina ya injini ya XT sasa inajumuisha injini bunifu ya Scania Super ya lita 13 yenye hatua ya utendaji ulioboreshwa ya 560 hp na kiwango cha juu zaidi cha hadi 8% cha kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji.

Nguvu inayotolewaTokiMafutaTeknolojia ya uchafuziPTO ya injini
770 Hp3700 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800 Nm
660 Hp3300 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800Nm
650 Hp3300 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800Nm
590 Hp3050 NmBiodizeli/Dizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800Nm
580 Hp3000 NmBiodizeli/Dizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800Nm
530 hp2800 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800Nm
520 hp2700 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)800Nm

Nguvu inayotolewaTokiMafutaTeknolojia ya uchafuziPTO ya injini
560 Hp2800 NmDizeli/HVOSCR MbiliHadi 1000 Nm
500 Hp2650 NmDizeli/HVO/FAMESCR MbiliHadi 1000 Nm
460 Hp2500 NmDizeli/HVO/FAMESCR MbiliHadi 1000 Nm
420 Hp2300 NmDizeli/HVOSCR MbiliHadi 1000 Nm

Nguvu inayotolewaTokiMafutaTeknolojia ya uchafuziPTO ya injini
540 Hp2700 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
500 Hp2550  NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
450 Hp2350 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
410 Hp2150 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
410 Hp2000 NmGESIKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)600 Nm
370 Hp1900 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm

Nguvu inayotolewaTokiMafutaTeknolojia ya uchafuziPTO ya injini
360 Hp1700 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
340 Hp1600 NmGesiKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)600 Nm
320 Hp1600 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
280 Hp1400 NmDizeli/HVOSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
280 Hp1350 NmGesiKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)600 Nm

Nguvu inayotolewaTokiMafutaTeknolojia ya uchafuziPTO ya injini
280 Hp1200 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
250 Hp1100 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm
220 Hp1000 NmDizeli/HVO/BiodizeliSelective Catalytic Reduction (SCR)600 Nm

Pata giaboksi sahihi

Aina zetu nyingi za giaboksi zinaweza kutumika kwa aina zote za usafiri. Kwa uendeshaji ulioboreshwa, giaboksi zetu za gia 8 na 12 zinaweza kuwekwa na mfumo wa Scania Opticruise na Scania Retarder.

Gia 8

Ubora wa giaboksi hii unapatikana katika urahisi wake. Zikiwa thabiti na imara, hakuna uwiano wa gia na utendakazi bora na laini unafanya iwe rahisi kubadilisha gia. Chaguo zinajumuisha Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania, Kidhibiti Mwendo cha Scania na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati.

Gia 8+1

Giaboksi hii inatoa manufaa sawa, pamoja na uwiano wa ziada wa gia. Kulingana na giaboksi ya kasi 4, pamoja na mipini ya kuingiza na kutoa nishati iliyolinganishwa, nguvu zake haziwezi kulinganishwa na nguvu za kiwango cha juu za uzungushaji za injini yoyote ya ndani ya Scania. Chaguo zinajumuisha Kidhibiti Mwendo cha Scania na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati.

Gia 12

Giaboksi hii imebuniwa ili kukabiliana na mandhari magumu zaidi, hali ambayo inafanya iwe chaguo bora zaidi kwa safari ya masafa marefu zaidi. Uwiano wake wa karibu zaidi wa gia unaunganisha wepesi na urahisi wa uendeshaji na gharama ya chini zaidi ya matumizi.

Gia 12+2

Kwa shughuli ambazo zinahitaji kasi ya chini zaidi ya uendeshaji, giaboksi hii ina gia mbili ziada. Ikiwa imebuniwa ili kupunguza gharama za matumizi, imethibitishwa kuwa fanisi zaidi kwa usafiri wa masafa ya mbali na ya karibu, pamoja na kwa kazi nzito za ujenzi. Gia za kupunguza kasi ya injini zinatoa uwezo wa juu wa nguvu za kuzungusha, pamoja na kupunguza kasi ya mizunguko ya chini na ya kupunguza gharama. Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania na Kidhibiti Mwendo cha Scania, pamoja na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati, inapatikana kwa ajili ya giaboksi zote za kugawanya gia.

Mfumo wa Scania Opticruise, unaopatikana katika hatua za utendaji za G25 na G33, unaweka kiwango cha sekta cha utendaji wa giaboksi kupitia matumizi bora zaidi ya mafuta, uthabiti wa kiufundi na uendeshaji.

 

Mfumo wa udhibiti wa klachi wa kiotomatiki wa Opticruise, wenye klachi ya ziada inayohitajika zaidi kwa uendeshaji bora, huwezesha usahihi wa uendeshaji na mbinu ya ubadilishaji wa gia inaoweza kubadilishwa kulingana na shughuli yaani, uzito wa gari na mteremko wa barabara. Hali huwezesha ubadilishaji bora na wa haraka wa gia, pamoja na udhibiti na starehe bora zaidi, katika kila hali ya uendeshaji. 

Kiwango pana na fanisi zaidi cha usambazaji wa nishati cha gia 14 cha mfumo wa Opticruise, ikijumuisha chaguo za gia za uwiano wa juu zaidi wa kasi ya kigurudumu na uwiano wa juu wa kasi ya uendeshaji, huchanganya uwezo bora zaidi wa kuwaka na matumizi bora zaidi ya mafuta. Hali hii inachangiwa na utendaji ulioboreshwa wa kurudi nyuma na chaguo la hadi gia 8 za kurudi nyuma, hatua ambayo inawezesha kurudi nyuma kwa kasi ya juu kwa mahitaji mahususi ya kazi.

Kando na kupunguza zaidi viwango vya utoaji wa kelele, mfumo wa Opticruise pia una muundo mpya na thabiti wa kijiometri na chumba cha giaboksi kilichotengenezwa kwa aluminiamu, hali ambayo inapunguza uzito wa kifaa wa hadi kilogramu 75.

 

Kupitia uthabiti wa kiufundi ulioboreshwa, vipindi virefu vya ubadilishaji wa oili na mahitaji machache ya kufanya matengenezo, mfumo wa Opticruise unahakikisha biashara endelevu bora zaidi katika hata mahitaji magumu zaidi ya kazi. 

Giaboksi mpya ya G33 ya Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania inapatikana kwa ajili ya injini zote za V8 za hadi 660 hp pamoja na injini za utoaji wa nishati ya kiwango za lita 13 za hp 500 na 540.

Gia za ekseli ya nyuma

Masafa ya ekseli ya nyuma ya Scania hutoa muundo thabiti na ulioboreshwa kwa uzito na aina mbalimbali za gia na uwiano, ili uweze kupata suluhu mwafaka kwa uendeshaji wako. Gia zote huja na kufuli vya difrensha.

Ekseli moja ya kuendesha yenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi

Gia zetu za kifaa kimoja cha kupunguza kasi zina kiwango cha chini cha mbano na utendaji wa kiwango cha juu na zinaweza kudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 78 na uwiano mkubwa wa gia kuanzia 1.95 hadi 5.57.

Ekseli ya kuendesha hebu yenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi

Ekseli za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi zinapatikana kwa ajili ya shughuli ambazo uwezo wa kuwashwa, nafasi kati ya fremu ya gari na barabara na kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa vinafaa. Hudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari kinachoruhusiwa cha hadi tani 80 na uwiano wa gia wa kuanzia 3.80 hadi 7.18.

EKSELI MBILI ZA KUENDESHA ZENYE KIFAA KIMOJA CHA KUPUNGUZA KASI

Ekseli mbili za kuendesha zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi zinatolewa kwa shughuli ambazo unahitaji kuvuta mizigo na matumizi ya kiwango cha chini cha mafuta. Gia ya kushuka ya RB662 + R660 hudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 80 na uwiano wa gia wa kuanzia 2.92 hadi 4.88.

Ekseli mbili za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi

Aina zetu nyingi za ekseli mbili za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi ni thabiti na za kudumu na zinatoa huduma bora zaidi ya kuwashwa kwa injini na nafasi kubwa kati ya fremu ya gari na barabara. Hudhibiti kiwango cha juu sana cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 210 na uwiano wa gia wa kuanzia 3.52 hadi 7.63.

Scania Modular Architecture Chassis

Mashine zako zinahitaji muundo wa chesisi ambao unaweza kustahimili hata changamoto ngumu zaidi za kazi. Scania Modular Architecture Chassis ambayo ni thabiti na inayoweza kubadilika kwa urahisi zaidi na aina ya tanki vimeundwa kwa njia maalum ili kutimiza mahitaji hayo. Hali hii inakupa fursa zaidi za kubainisha na kutumia lori lako la Scania kwa njia ambayo inafaa zaidi kwa kazi yako, pamoja na kuboresha usambazaji wa uzito wa chesisi, uzito wa gari na hata aina za matumizi.

Katika moyo wa XT

Kuwa sehemu ya msururu wa uzalishaji kunamaanisha kutegemea wengine kila wakati, kama vile wengine watakutegemea wewe kila wakati. Kwa uwiano wa juu wa toki-hadi-farasi wa injini zote za Scania, safu ya XT imeandaliwa kwa misheni yoyote iliyo mbele. Kutoka kwa injini nyepesi ya lita 7 hadi Scania V8 maarufu, tunatoa anuwai ya njia mbadala za injini.

INJINI ZENYE NGUVU

Injini za magari ya Scania zinajulikana kwa matumizi bora ya mafuta. Malori yetu yanachukua sifa yetu hatua zaidi. Sindano zilizoboreshwa, vyumba vya mwako na uwiano wa ekseli ya nyuma, vyote huchangia kupunguza kasi ya injini na kupunguza matumizi ya mafuta kwa 3%.

 

Mpangilio wa ekseli

Ekseli ya mbele, nyuma, isiyozunguka na inayozunguka – Scania inaweza kutimiza mahitaji ya shughuli yoyote. XT inaweza kuunganishwa na anuwai ya usanidi wa chasi yenye urefu tofauti.

4x2
Kimo cha chesisi
Chini zaidi, chini, kawaida, juu

4x4

Kimo cha chesisi
High

6x2
Kimo cha chesisi
Kawaida

6x2/2
Kimo cha chesisi
Kawaida

6x2 ya kusukuma

6x2/4

Kimo cha chesisi
Kawaida, fupi
6x2 inaendeshwa na ekseli mbili

6x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu

6x6
Kimo cha chesisi
High

4x2
Kimo cha chesisi
Chini, kawaida, juu

4x4
Kimo cha chesisi
High

6x2
Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida

6x2/2
Kimo cha chesisi
Kawaida

6x2 ya kusukuma

6x2/4

Kimo cha chesisi
Kawaida
6x2 inaendeshwa na ekseli mbili

6x2*4

Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida

6x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu

6x6
Kimo cha chesisi
High

8x2
Kimo cha chesisi
Kawaida

8x2*6

Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida

8x2 inaendeshwa na ekseli ya nyuma

8x2/4

Kimo cha chesisi
Kawaida

8x2 inaendeshwa na ekseli mbili

8x4

Kimo cha chesisi
Kawaida, refu

8x4*4

Kimo cha chesisi
Kawaida

8x4 inaendeshwa na ekseli ya nyuma

10x4*6

Kimo cha chesisi
Kawaida

10x4 inaendeshwa na ekseli ya nyuma

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Pata tawi letu lililo karibu na wewe.
Call us
E-mail us
E-mail Workshop
View Dealer Website
OPENING HOURS
ACCEPTED CREDIT CARDS

Bidhaa zetu mbali mbali