Sifa
Sekta ya uchukuzi inabadilika haraka, na ili kuendesha mabadiliko kuelekea suluhisho safi, salama na nadhifu, tunahitaji kuzingatia maeneo sahihi. Kwa kuchanganya nguvu zetu za msingi - kama vile jukwaa la kawaida la Scania - na njia mpya za kufanya kazi, tunakuza mawazo na teknolojia kwa haraka ambazo zitaboresha mfumo wa usafiri wa kesho.
-
-
-
-
-
Utengenezaji wa magari ya kielektroniki
15 Apr 2022 Udumishaji ni kipaumbele cha juu katika kampuni ya Scania na kubadilisha teknolojia za kutumia mafuta na kuanza kutumia teknolojia za umeme kama chanzo cha nishati ni sehemu muhimu ya kudumisha sekta ya usafiri. Mabadiliko ya kuacha kutumia teknolojia za kutumia mafuta na kuanza kutumia teknolojia za kutumia umeme kama chanzo cha nishati yanatendeka kwa kasi na kampuni ya Scania ina mpango wenye mbinu nyingi wa kuwezesha usafiri unaotumia umeme, ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti wa aina mbalimbali za teknolojia mseto za kutumia mafuta yasiyotoa gesi ya kaboni na magari ya kutumia umeme pekee. Tumetoa ahadi ya kuzindua gari jipya la kutumia umeme kila mwaka kuanza sasa. -
-
Usalama
28 Jan 2022 Katika Scania, tunaendelea kufanya kazi ili kuboresha usalama wa magari yetu. Shukrani kwa vizazi vya utafiti wa kina, muundo na majaribio, magari ya Scania yamethibitishwa kuwa salama ya kipekee. Tembelea tovuti yetu ili kuona jinsi tunavyoweza kukuweka salama ndani ya sekta ya usafiri.