Tanzania

Huduma ya Usaidizi ya Scania

Tuko nawe kila wakati

Popote ulipo, Huduma ya Usaidizi ya Scania inapatikana kila wakati – simu yako itapokelewa mara moja na mratibu wa huduma ambaye ni mtaalamu anayefahamu vyema gari lako la Scania – na anayezungumza lugha yako. Kwa hivyo, gari lako likipata hitilafu, kuna mtu aliye tayari kila wakati kukusaidia.

Hutambua tatizo

Tutakufahamisha jinsi ambavyo tunaweza kukusaidia na kadirio la muda ambao tutachukua. Panapohitajika, tutatuma gari la kutoa huduma – na vipuri vinavyofaa kwa gari lako na zana sahihi - mahali ulipo. 

Endelea na kazi yako

Timu yetu itaharakisha mambo kwa kuweka muda unaokadiriwa kwa matengenezo na dhamana au kufanya ukaguzi wa maelezo ya malipo kwa niaba yako. Ikiwa huduma nyingine zinahusishwa, tutahakikisha kuwa huduma sahihi inatolewa kwa wakati unaofaa ili uweze kuendelea na kazi yako.

Hufanya mpango

Hitilafu nyingine hutokea mahali pasipotarajiwa au huhitaji muda mwingi ili kusuluhishwa. Tutasaidia kuweka mpango wa kukupa gari la kutumia kwa muda mfupi na kukupa huduma za malazi au usafiri.

Nambari ya huduma ya dharura

Huduma ya Usaidizi ya Scania inapatikana kila wakati. Piga tu simu kwa nambari 0800 800 660 au 0044 1274 301260 ukiwa nje ya nchi. Ili kuharakisha mambo, hakikisha uko tayari na nambari ya fremu ya gari, namabri ya usajili na maelezo ya mahali ulipo.

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Pata tawi letu lililo karibu na wewe.
Call us
E-mail us
E-mail Workshop
View Dealer Website
OPENING HOURS
ACCEPTED CREDIT CARDS