Mabasi ya jiji na mabasi ya usafiri wa umma
Kwa kila maili na kwa kila safari
Kampuni ya Scania inalenga kuwa katika mstari wa mbele wa kutoa huduma thabiti ya usafiri. Na tunafahamu kuwa kujali suala nzima kunahitaji kuweka juhudi nyingi katika huduma zetu. Kwa zaidi karne mmoja, tumeelewa na kupata maarifa ya kina ambayo yanatuwezesha kutengeneza mabasi ya usafiri wa mijini, mabasi ya usafiri wa umma na huduma zinazohitajika ili kutoa huduma thabiti za usafiri – kila mahali.
Katika kampuni ya Scania, tunakabiliana na changamoto kutoka pembe zote, kwa kutengeneza aina nyingi za magari yenye ubora wa juu na huduma mahiri ambazo zinaruhusu uthabiti kwenda sambamba na uchumi uliopo. Hivyo ndivyo tunaamini kuwa tunaleta mabadiliko ya kweli.
Magari yaliyotengenezwa ili kufaa mahitaji maalum
Magari yaliyobuniwa hasa kutekeleza shughuli zisizo za kawaida au kutimiza masharti makali sana. Kampuni ya Scania ina mabasi kadhaa duniani kote yaliyotengenezwa ili kutimiza mahitaji haya, kulingana na hali kutegemewa, kudumu na utendaji.
Basi la kusafirisha abiria na mizigo
Kando na kusafirisha abiria, basi hili pia hubeba mizigo kwenye sehemu ya kubeba mizigo katika upande wa nyuma. Limeunda kwa muundo wa lori la kusambaza mizigo. Lina mfumo wa kurekebisha hewa na lifti ya upande wa nyuma ya kupandisha na kushusha mizigo.
Basi la wagonjwa
Basi hili lililoundwa kwa teknolojia ya juu lina vifaa vya matibabu vya kuhudumia wagonjwa mahututi. Limetengenezwa kwa njia maalum na lina nafasi ya madaktari kuhudumia wagonjwa.
Basi la kupanda milima
Basi fupi ambalo lina nafasi ndogo kati ya fremu na barabara na injini yenye nguvu zaidi, limebuniwa kwa njia maalum ili kufaa kuendeshwa kwenye mandhari magumu katika milima ya Uswisi; barabara nyembamba yenye kona kali, miteremko mikali, barabara duni na hali mbaya zaidi za hewa.
Kituo cha kuchangisha damu
Basi hili ni kituo cha kuchanganisha damu kinachosonga ambalo lina vifaa vinavyohitajika kwa shughuli ya kuchangisha damu.