L-Msururu
Gari fupi la teksi
Malori mafupi yanayofaa kwa shughuli za mjini
Kama vile tu biashara yako ilivyo ya kipekee, ndivyo lilivyo jiji ambako unafanya kazi. Uendeshaji wa magari mjini unahusisha hali nyingi za kuendesha na kusimama, kupanda na kushuka mara kwa mara, na kuhitaji kuendelea kufuatilia magari mengine na wapita njia walio karibu na lori unapoendesha.
Gari la Scania L-series limeundwa kwa kuupa usalama kipaumbele cha msingi na limeundwa ili kufaa kwa shughuli nyingi katika hali ngumu zaidi za jiji. Gari la teksi la L-series lina sehemu ya ndani ya starehe na sehemu thabiti za nje. Urahisi wa kufikia sehemu nyingine za ndani, urahisi wa kupiga magoti na uwezo wa kuona ulioboreshwa inafanya iwe rahisi na haraka kuingia na kutoka kwenye gari.
Usalama umehakikishwa. Limeundwa kwa starehe.
Limeundwa ili kufaulu na kupita katika mazingira ya kasi ya juu, urahisi wa kufikiwa inafanya iwe rahisi kuingia na kutoka, huku pia ikiwa rahisi kutembea katika sehemu za ndani. Ufanisi, usalama na starehe vyote katika kifurushi kimoja bora zaidi.
Limeundwa ili kufaa kwa mazingira ya mjini
Gari la teksi la L-series liliundwa ili kufaulu katika mazingira magumu zaidi ya mjini na limeboreshwa ili kuunda mazingira bora zaidi ya kazi iwezekanavyo na uwezo wa kuona moja kwa moja.
Haya yote bila kuathiri uthibitishaji wa uthabiti wakati wa ajali na usalama unaotarajia kutoka kwa magari makubwa ya teksi.
Ufikiaji wa sehemu za ndani za gari
Gari la Scania L-series lina uwezo bora zaidi wa kufikia sehemu za ndani za gari. Dambra iko chini na mbele zaidi kwenye chesisi na sehemu ya injini haizuii njia. Hii inafanya iwe rahisi kwa dereva kupanda na kushuka kupitia pande zote za gari.
Gari la L-series lina sehemu pana ya wafanyakazi na ufanisi na utendakazi wa juu.
Kufikia kwa urahisi
Ngazi pana za kupanda za upana wa 790 mm pamoja na mlango wa kufunguka kwa upana zaidi inahakikisha unaingia na kutoka kwa starehe.
Pia, sehemu ya kupiga magoti ya teksi (kawaida katika matoleo ya hatua moja na inapatikana kama chaguo la matoleo ya hatua mbili) inafupisha mwinuko kwa 100 mm wakati breki ya kuegesha inashikwa. Hii inapunguza matumizi ya nguvu nyingi kwa kuwezesha kuingia kwa mwendo wa taratibu.
Dirisha salama la jiji
Dirisha Salama la Jiji (City Safe Window) la Scania ni dirisha la mlango la chini ambalo linampa dereva uwezo wa kuona vizuri wapita njia na waendeshaji baiskeli walio karibu, pamoja na umakinifu mzuri katika hali za shughuli nyingi za mjini.
Dirisha hili linafanya iwe rahisi kuendesha gari katika mazingira ya msongamano mkubwa na linasaidia kuzuia ajali kwa kupanua sehemu ya kuona.
Mlango wa jiji
Mlango wa Jiji wa Scania unafanya gari la teksi la L-series kuwa fanisi hata zaidi katika shughuli ambapo wafanyakazi huingia na kushuka mara kwa mara wakati wa siku ya kazi, na kuwawezesha kuona vizuri kilicho nje karibu sana na teksi.
Hali ya mlango kufunguka ukielekea ndani inamaanisha inawezekana kushuka kwenye teksi kwa usalama katika upande wa abiria kwenye barabara za shughuli nyingi, au kushuka katika nafasi ndogo zaidi kama vile likiwa limeegeshwa karibu na ukuta au ua.
Nafasi ya hadi viti vitatu vya abiria
Tunajua kwamba shughuli nyingine zinahitaji kuwepo kwa wafanyakazi wachache kwenye gari ili kuboresha ufanisi katika mazingira magumu zaidi ya mjini.
Gari la L-series linaweza kuwekwa hadi viti vitatu vya abiria, kuweka viti viwili vya ziada katikati ya gari ili kuunda nafasi inayohitajika ya kubeba watu wanne kwenye teksi, huku bado ikiwezesha kila mtu kusafiri kwa starehe na kufanya kazi ipasavyo.
Chaguo za teksi za L-series
Magari ya L-series yanapatikana katika chaguo tatu za kipekee za teksi, kila mmoja na faida zake za kipekee ili kulingana na mahitaji ya aina tofauti za shughuli. Imejumuishwa pia kikamilifu katika mfumo wa moduli wa Scania, hatua inayoruhusu vifuasi na vipuri kubadilishwa kwa urahisi kulingana na matumizi yako maalum.
Teksi ya chini ya L-day
Teksi ya chini zaidi katika aina ya L-series ni chago bora wakati jumla ya urefu wa chini ni kipaumbele, kwa mfano ili kuingia na kuondoka kwenye gereji, au wakati unaendesha katika viwanja vya ndege.
Urefu wa Teksi
2,700 mm (bila vipunga upepo)
Kitanda
Hakuna
Mfumo wa kusambaza nishati
280-360 hp
Teksi ya kawaida ya L-day
Teksi ya ukubwa wa wastani katika aina ya magari ya L-series bado ina jumla ya urefu wa chini wa teksi lakini pia inaruhusu viti viwili vya ziada kuwekwa kwenye sehemu ya injini na kuwezesha kubeba abiria watatu.
Urefu wa Teksi
3,040 mm (bila vipunga upepo)
Kitanda
Hakuna
Mfumo wa kusambaza nishati
280-360 hp
Teksi ndefu ya L-day
Teksi ya starehe zaidi yenye chumba cha ziada cha hifadhi na chumba cha ziada cha wafanyakazi, inayorahisisha hata zaidi kutembea ndani ya teksi.
Urefu wa Teksi
3,300 mm (bila vipunga upepo)
Kitanda
Hakuna
Mfumo wa kusambaza nishati
280-360 hp
Kuboresha shughuli zako za kila siku
WIKAB, kampuni ya Uswidi inayofanya kazi na usalama wa barabarani, iliboresha mazingira yake ya kazi kwa kuchagua teksi fupi ya Scania kwa ajili ya lori lao la TMA.
Uwezo wa kuona moja kwa moja
Gari la L-series lina nafasi ya chini ya kuendeshea, inayomweka dereva katika urefu sawa kama watu wengine walio karibu na gari.
Dashibodi ya chini na kizingiti cha dirisha na vijenzi thabiti vya kioo na mihili miembamba ya A inaboresha uwezo wa dereva wa kuona kwa asilimia 12, na kupunguza hatari ya kutokea kwa ajali na kupanua sehemu ya kuona ya dereva wako.
Mazingira ya kazi
Teksi zetu na springi za teksi zimeundwa ili kupunguza kelele na mitetemo ili kuongeza starehe.
Kiti cha dereva na usukani vinaweza kurekebishwa ili upate nafasi yako nzuri ya kuendesha. Gari la L-series lina pia utendaji bora zaidi wa uthabiti wakati wa ajali kwa usalama wa madereva.
Lori la jiji la kawaida
Maja Stomby, dereva wa majaribio ya nyanjani, anatathmini gari la L-series la Scania, teksi fupi za mazingira ya mjini. “Ni kama kuendesha gari nzuri bora zaidi la abiria,” anasema.
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.