Tanzania

Chesisi ya Scania K

Sakafu ya juu

Mitambo ya injini

Chesisi ya Scania K ya sakafu ya juu hutoa aina mbalimbali za mitambo ya injini yenye ufanisi wa nishati na za kuaminika zilizoboreshwa kwa trafiki ya mijini na mikoani.

InjiniNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 9320 Hp (235kW)1600 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Mota ya umeme130 kW1030 NmHakuna uchafuziUmeme

Giaboksi:
12-kasi na mashine jumuishi ya umeme

 

UjazoNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 7280 Hp (206 kW)1200 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 9280 Hp (206 kW)1400 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)HVO, Dizeli
Lita 9320 Hp (235 kW)1600 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 9360 Hp (265 kW)1700 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 13370 Hp (265 kW)1900 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)HVO, Dizeli
Lita 13410 Hp (302 kW)2150 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Ujazo wa mafuta:
Lita 275 - 460 , lita 450 - 560 (ya muunganisho)
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania
Injini za lita 13 zenye kutoa nguvu zaidi pia zinapatikana chini ya Chesisi ya basi.

UjazoNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 9280 Hp (206 kW)1350 NmKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)Biogesi, Gesi asili
Lita 9340 Hp (250 kW)1600 NmKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)Biogesi, Gesi asili

Ujazo wa mafuta:
Lita 1260 hadi 1875
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

Ekseli

Chesisi ya Scania yenye sakafu ya juu inapatikana katika anuwai kadhaa kuiwezesha kukidhi mahitaji tofauti ya uendeshaji.

4x2 - ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu

6x2 - viangiko huru au ekseli iliyo imara

6x2*4 - ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu

6x2/2 - (ARTIC) Ekseli thubutu

Kiwango cha sakafu

Basi lina sakafu bapa ambayo inafikiwa kupitia ngazi unapopanda. Ghorofa ya juu inaboresha starehe ya abiria, maoni na uwezekano wa nafasi ya mizigo.

Vipengele vya muundo

Chesisi ya Scania K yenye sakafu ya juu inakidhi mahitaji ya waendeshaji katika kila bara. Kwa udhibiti kamili wa ubunifu na utengenzaji wa fremu na mfumo wa uendeshaji, kampuni ya Scania inatengeneza fremu za kutegemewa, za kudumu na za utendaji bora wa kipekee.

 

Fremu ya chesisi

Ekseli ya mbele iliyoimarishwa inamaanisha kuwa uwezo wa mzigo umeongezeka kutoka tani 7.5 hadi 8.2. Hii inaruhusu uwezo wa juu wa kubeba mzigo. Hali hii pia inawezesha usambazaji bora wa uzito kati ya ekseli za mbele na nyuma, ambalo ni jambo la muhimu kwa magari ya umeme na yanayotumia mafuta. Zaidi, uzito wa chesisi umepunguzwa kwa 2% (>>100kg) bila kuathiri uimara, na hivyo kuchangia kupunguza matumizi ya mafuta.

Teknolojia ya nguvu za injini

Mifumo ya uendeshaji inaotegemewa zaidi, inayodumu na thabiti inawezesha hatua ya kuokoa mafuta kwa hadi 21%, hali ambayo inawezeshwa kupitia vigezo kadhaa kama vile; ubora wa injini (-6%), giaboksi iliyoboreshwa (-3%), kupunguzwa kwa uzito (-3%) na kuongezwa kwa kipengele cha kuwasha/kuzima (-6%).

Mfumo ya umeme

Usanifu mpya wa usambazaji wa nishati unakuja na vitengo vilivyoboreshwa vya udhibiti wa kielektroniki (ECUs) na utendaji ambao huboresha utendakazi na kuwezesha uchunguzi kwa ukarabati na matengenezo. Pia huwezesha utendakazi mpya ndani ya ADAS, uhamaji wa kielektroniki na mifumo ya usafiri unaojiendesha.

Udhibiti wa joto la betri

Inashughulikiwa na mfumo wa kupozea maji uliofungwa ambao, katika halijoto ya mazingira ya kupita kiasi, husaidiwa na kipazajoto cha umeme au kupoezaji cha AC mtawalia. AC hii imeunganishwa katika saketi ya kupoeza betri lakini imetenganishwa na AC ya abiria na dereva, na kusababisha mazingira ya abiria yasiyoathiriwa.

Eneo la dereva

Hutoa egonomiki bora kupitia marekebisho yote ya kiti cha kisicho na ngazi, paneli ya ala inayoweza kubadilishwa, uwekaji wa swichi unaonyumbulika . Paneli ya ala iliyo chini kiasi huongeza mwonekano. Mabasi hayo yana uwezo bora zaidi wa kuendesheka na yana eneo kubwa la kugeuza, mifumo ya hali ya juu ya usaidizi wa madereva, na ushughulikiaji ulioboreshwa wa kusaidiwa, usukani na breki. Pia, hutoa usalama ulioongezeka, mfumo bora wa hali ya hewa na mfumo mzuri wa kupunguza kelele na mitikisiko.

Teknolojia ya viangiko vya mbele

Bila kuathiri uwezo wa kubeba abiria, viangiko vipya kwa mbele vya kujitegemea vinatoa starehe bora. Viangiko vipya vya mbele imara pia huongeza uwezo wa kubeba abiria na hutoa starehe nzuri pamoja na njia pana na ya chini ya basi ya sitahani mbili.

Endelea kuchunguza

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Pata tawi letu lililo karibu na wewe.
Call us
E-mail us
E-mail Workshop
View Dealer Website
OPENING HOURS
ACCEPTED CREDIT CARDS