Tanzania

Scania Citywide

Fremu fupi

Mitambo ya injini

Scania Citywide yenye muingilio wa chini inatoa aina mbalimbali za treni za ufanisi wa nguvu na za kuaminika zilizoboreshwa kwa trafiki ya ndani ya jiji na miji.

InjiniNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 9320 Hp (235kW)1600 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Mota ya umeme130 kW1030 NmHakuna uchafuziUmeme
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

UjazoNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 7280 Hp (206kW)1200 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 9280 Hp (206kW)1400 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)HVO, Dizeli
Lita 9320 Hp (235 kW)1600 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 9360 Hp (265 kW)1700 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Ujazo wa mafuta:
Lita 140 hadi 360, lita 450 hadi 560 (imeunganishwa)
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

UjazoNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 9280 Hp (206 kW)1350 NmKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)Biogesi, Gesi asili
Lita 9340 Hp (250 kW)1600 NmKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)Biogesi, Gesi asili

Ujazo wa mafuta:

Lita 1260-1875
Giaboksi:

Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

Ekseli, milango, urefu

Scania Citywide yenye kiingilio cha chini inapatikana katika matoleo tofauti na chaguo kadhaa za usanidi wa milango ili kuweza kukidhi mahitaji tofauti ya uwezo na mtiririko wa abiria.

Juu

Kimo cha Scania Citywide kinategemea uchaguzi wa kiendeshaji, na matanki ya gesi na vipengele vya umeme vilivyowekwa kwenye paa.

3.19 m (mseto)
3.31 m (dizeli)
3.40 m (gezi)

Kiwango cha sakafu

Sehemu ya chini ya kuingilia na sakafu bapa hadi kwenye sehemu ya milango ya katikati inatoa uwezo sawa wa kufikiwa kama wa toleo la sakafu ya chini katika sehemu za katikati na mbele. Katika sehemu nyuma, sakafu iliyoinuka inakuwezesha kuona vizuri abiria. Njia pana ya katikati inachangia urahisi zaidi wa ufikiaji, starehe na kupanda na kushuka kwa abiria.

Vipengele vya muundo

Scania Citywide yenye muingilio wa chini limeundwa na kutayarishwa na Scania. Kila kitu kutoka kwa ujenzi wa chesisi hadi mitambo ya nguvu ya uendeshaji na mwili imetengenezwa na kujaribiwa kikamilifu kwa kuzingatia kutegemeka na utendakazi bila kuathiri ufanisi wa nguvu.

Vipengele vya usalama

Mabasi ya Scania yana mifumo ya hali ya juu ya usaidizi wa madereva (ADAS) ikijumuisha onyo la kugongana kwa watumiaji wa barabara walio hatarini, onyo la mahali pasipoonekana, udhibiti wa kasi ya usafiri unaobadilika, usaidizi wa tahadhari, na breki za dharura za hali ya juu. Zaidi ya hayo, teknolojia ya breki ya maegesho ya nyumatiki huepuka mwendo wa basi bila kukusudia na hivyo basi ajali zinazoweza kutokea. Kupitia ujenzi wa miili iliyoimarishwa na chesisi, mabasi yetu yanajengwa kulinda abiria, madereva na vifaa nyeti.

Muundo wa nje

Muundo mpya wa kisasa na wa wa kistraarabu wa nje wa Scania Citywide unaashiria uvumbuzi, ubora na mawazo ya mbele. Ina umbo dogo na vifuniko vya paa vya vipengee kama vile vizio vya AC, tanki za gesi na pakiti za betri. Dirisha la chini huchangia kupunguza mipaka kati ya basi na mazingira yake. Zaidi ya hayo, ufikiaji rahisi wa vituo vya huduma na paneli za kona za nje zinazoweza kubadilishwa kwa urahisi huokoa muda wakati wa ukarabati na matengenezo.

Fremu ya chesisi

Ekseli ya mbele yenye nguvu zaidi, pamoja na uwezo wa kutumia magurudumu mapana kwa sasa, inamaanisha kuwa uwezo wa kubeba mizigo umeongezeka kutoka tani 7.1 hadi 8.2. Hali hii inaruhusu kubeba abiria wengi zaidi. Pia huwezesha usambazaji wa uzani ulioboreshwa kati ya ekseli za mbele na za nyuma, ambayo ni muhimu sana kwa magari ya gesi na umeme. Pia, uzito wa fremu umepunguzwa kwa asilimia mbili (2%) (>100 kg) bila kuathiri uthabiti, hali ambayo inachangia matumizi ya mafuta ya kiwango cha chini.

Teknolojia ya nguvu za injini

Mifumo ya uendeshaji inaotegemewa zaidi, inayodumu na thabiti inawezesha hatua ya kuokoa mafuta kwa hadi 21%, hali ambayo inawezeshwa kupitia vigezo kadhaa kama vile; ubora wa injini (-6%), giaboksi iliyoboreshwa (-3%), kupunguzwa kwa uzito (-3%) na kuongezwa kwa kipengele cha kuwasha/kuzima (-6%).

Mfumo wa kuongeza na kupunguza joto

Mfumo wetu bora zaidi wa kuongeza na kupunguza joto unapunguza matumizi ya nishati, bila kujali hali ya anga. Mfumo wa kuongeza joto hurudisha nishati kwenye mfumo hatua ambayo husababisha mzunguko wa hewa unaokoa nishati na udhibiti wa hali ya kuongeza na kupunguza joto. Mfumo wa kupunguza joto pia umetengwa kutoka kwenye mfumo wa uendeshaji, hatua ambayo inasababisha kuwepo kwa mazingira ya starehe kila wakati.

Dhana ya kukata-kwa-urefu

Urefu wa basi letu unaonyumbulika katika nyongeza za mm 100 huwezesha mipangilio iliyoundwa mahususi. Kila sehemu ya mwili ya mm 100 ni sawa na kilo 100 na uwezekano wa kuokoa mafuta ni 0.3%.

Endelea kuchunguza

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Pata tawi letu lililo karibu na wewe.
Call us
E-mail us
E-mail Workshop
View Dealer Website
OPENING HOURS
ACCEPTED CREDIT CARDS