Tanzania

Scania inawekeza kwenye kiwanda cha kuunganisha betri

Na upanuzi wa haraka wa aina mbalimbali za malori ya umeme ya Scania, mabasi na injini, kampuni inapanga, kwa miaka kadhaa ijayo, kuwekeza zaidi ya SEK bilioni 1 katika kiwanda cha kuunganisha betri huko Södertälje, Uswidi. Hatua ya kwanza ni jengo la ukubwa wa mita za mraba 18,000 na ujenzi utaanza mapema 2021 kwa lengo la kuanza kutumika kikamilifu ifikapo 2023.

"Hii ni dhihirisho dhahiri la azimio letu la kuchukua jukumu kuu katika uzalishaji wa magari makubwa ya umeme, ambayo inahitajika ili kutimiza dhamira yetu ya malengo ya hali ya hewa kutokana na sayansi," anasema Ruthger de Vries, Mkuu wa Uzalishaji na Utaratibu wa Usafirishaji katika Scania. "Kuendesha kiwanda cha kuunganisha betri katika eneo moja ni sharti la kimsingi katika uzalishaji wa kadiri kubwa wa magari ya umeme na pia inaimarisha nafasi ya Scania kama sehemu ya mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa betri."

 

Kiwanda na ambacho kitajengwa mkabala na kiwanda cha kuunganisha fremu huko Södertälje kitaunganisha moduli za betri na paketi kutoka kwa seli ambazo zitaletwa kutoka kiwanda cha betri cha Northvolt huko Skellefteå, Uswidi. Paketi zilizounganishwa huunda mifumo ya betri iliyoundwa kwa ajili ya uzalishaji wa moduli wa Scania. 

 

"Scania inaendelea kuwekeza katika eneo la Stockholm na kujenga uwezo mkamilifu wa kusambaza umeme. Usambazaji umeme utabadilisha usafiri na uwekezaji huu wa hivi punde zaidi katika shughuli za Scania huko Södertälje utaimarisha zaidi Uswidi kama kitou cha ubunifu wa hali ya juu ndani ya uwekaji umeme katika magari makubwa", anasema de Vries. 

 

Mnamo 2015, Scania ilianza uzalishaji wa mfululizo wa mabasi ya mahuluti na mnamo 2019 ya safu yake ya kwanza ya mabasi yanayotumia umeme kikamilifu. Hii ilifuatiwa hivi karibuni na kuanzishwa kwa lori mahuluti la kuunganishwa na umeme la Scania na lori linalotumia umeme kikamilifu. Uzalishaji wa mfululizo wa lori linalotumia umeme utaanza 2021. Wakati huo huo, suluhu zinazotumia umeme za viwandani na baharini zinatengenezwa. Scania sasa itaongeza uzalishaji polepole, ambao umejikita huko Södertälje.

 

Huku ikiajiri wafanyikazi 200, wengi wakiandikishwa kutoka ndani ya kampuni, kiwanda cha kuunganisha betri kitajiendesha kiotomatiki kutoka kwa bidhaa zinazoingia kupitia uzalishaji hadi utoaji. Wafanyakazi wa kushughulikia viungo vya kuzalishwa kwa mikono vya muunganisho wa moduli za betri, kama vile kuweka viungo vya kebo, watafunzwa usalama wa umeme na kujikinga.

 

Paketi za betri zitaundwa mahsusi kwa matumizi tofauti na kuwasilishwa kwenye kiwanda wa chesisi kilichoko karibu, ambayo kwa sasa kinapangwa upya kwa uunganishaji sambamba wa magari ya umeme na magari ya injini za mafuta.